array(0) { } Radio Maisha | Justin Muturi kuteuliwa kuwania nyadhifa wa Naibu wa Rais mwaka 2022.

Justin Muturi kuteuliwa kuwania nyadhifa wa Naibu wa Rais mwaka 2022.

Justin Muturi kuteuliwa kuwania nyadhifa wa Naibu wa Rais mwaka 2022.

Wazee wa jamii ya Embu wamewataka wenzao wa Kikuyu kuwaunga mkono katika harakati za kumshinikiza Naibu wa Rais William Ruto kumteua Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi kuwa mgombea mwenza mwaka wa 2022.

Wakizungumza katika eneo la Siakago, wazee hao aidha wamesema kwamba wamekuwa wakiwaunga mkono wenzo wa jamii ya Kikuyu kwa muda hivyo wakati umewadia wa kiongozi kutoka Embu kuungwa mkono.

Naibu Kiranja katika Bunge la Kitaifa, Sicily Mbarire kwa upande wake ametangaza kwamba viongozi wa Embu watazunguka kote nchini kumpigia debe Spika Muturi.

Ikumbukwe baadhi ya viongozi wa eneo la Kati wanapendekeza Seneta wa Tharaka Nithi, Kindiki Kithure kuwa mgombea mwenza wa Ruto.

Mwingine anayepigiwa debe ni Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru.