array(0) { } Radio Maisha | Uzinduzi wa Mashine ya M-Pima itakayowasaidia wanaoishi na HIV
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Uzinduzi wa Mashine ya M-Pima itakayowasaidia wanaoishi na HIV

Uzinduzi wa Mashine ya M-Pima itakayowasaidia wanaoishi na HIV
Kwa muda mrefu mikakati imewekwa kukabili virusi vya HIV, K wa kuazishwa kwa tembe za kumaliza makali hayo ARV's, watoto kuzaliwa bila virusi hivyo hata mama akiwa navyo na wanandoa kuishi bila kuambukizana hata mmoja akiwa na virusi hivyo. Katika juhudi hizo  Shirika la Utafiti wa Afya ABBOT limezindua mashine itakayo saidia pakubwa katika kujua viwango vya virusi HIV vilivyo katika damu yaani Viral load kwa muda wa dakika sabini kinyume na hapo awali ambapo ilichukua muda usiopungua wiki mbili.
 
Watu walio na virusi vya HIV ambao wanaoishi maeneo kame au maeneo yaliyo mbali na hospitali au zahanati wamekuwa wakiathirika pakubwa kupata matibabu na kujua viwango vya virusi HIV vilivyo katika damu zao yaani Viral load , kwani unapopimwa viwango hivyo utasubiri kwa muda wa wiki mbili au zaidi kupata majibu.
 
Dakta Kuku Appiah  Mkurugenzi wa ABBOT wa Afrika wa Masuala ya tiba na Sayansi Abbot amesema hali hiyo imerahisishwa baada ya Shirika la Afya Dunia WHO,Mwezi Aprili mwaka huu kuidhinisha matumizi ya kifaa kiitwacho M-PIMA cha kupima viwango vya virusi hivyo katika damu. Kuidhinishwa kwa WHO kumesaididia pakuubwa kwani matokeo ya M-PIMA hutoka baada ya dakika sabini.
 
 
Vilevile Dakta Appiah ameeleza kuwa si lazima wahudumu wa afya wawe na ujuzi wa maabara ili waweze kutumia M-PIMA, jambo amablo limerahisisha utoaji wa majibu hasa katika maeneo yaliyo na wahudumu wa afya wachache.
 
Mpango wa 90-90-90 goals ulioanzishwa na Shirika la UNAIDS , ukilenga kufikia mwaka 2020, mataifa yote duniani yahakikishe asimilia 90 ya walio na virusi vya HIV wanajua hali yao, asilimia 90 ya walio na HIV wantumia tembe za ARV'S na makali ya asilimia HIV ya mepunguzwa kwa asilimia 90 walio na virusi hivyo.
 
Baada ya kuziduliwa kwa M-PIMA wengi walitaka kujua iwapo wanaweza kutumia mashine hizo wenyewe nyumbani, jambo ambalo Dakta Apiah amepinga kisistiza kuwa uchunguzi wa kujua viwango vya HIV huwa baada ya wiki 2 hadi 4 unagundua una virusi hivyo kisha kati ya miezi mitatu na na minne hadi wakati viwango hivyo vitapunguzwa kabisa.
 
Utafiti uliofanywa na Shirika la Healthy Nation mwaka jana unaonyesha kuwa takriban Wakenya milioni 1.4 wanaishi na virusi vya HIV. Huku visa vipya vya maambukizi vikiwa takriban 52,00 kutoka elfu mia moja mwaka wa 2014.
 
Takriban vijana 184, 719 waliokati ya miaka 15-24 wanaishi na virusi vya HIV. Huku baadhi wakilalamika kuchoshwa na dawa hizo.Hata hivyo wahudumu wa afya wamesisitiza matumizi ya dawa hizo ili kupunguzza makali ya HIV, kuzuia maambukizi, na kumwezesha aliye na HIV kuishi maisha ya kawaida.