array(0) { } Radio Maisha | Melon na Sharon ni pacha

Melon na Sharon ni pacha

Melon na Sharon ni pacha

Sharon Lutenyo na Melon Mathias,  pacha fanani, Identical Twins ni madada, umebainisha  uchunguzi wa msimbojeni, DNA uliofanywa na madaktari katika Maabara ya Lancet Kenya. Aidha familia hizo zimesema kwamba matokeo hayo hayatawatenganisha pacha hao.

 Uchunguzi huo uliofanywa baada ya mapacha hao kupewa ushauri nasaha , umethibitisha kwamba Mevice Imbaya ni mtoto wa Angeline Omina na Wilson Lutah.

Kwa mujibu wa maabara hiyo, kila mmoja alifanyiwa uchunguzi wa chembechembe za damu kivyake kisha kufananishwa. Uongozi wa Lancet Kenya,  unasema kwamba uchunguzi wa DNA unagharimu pesa nyingi ila wasichana hao walipata ufadhili.

Kwa mujibu wa familia hizo mbili, matokeo hayo hayatawatenganisha wasichana hao watatu.

Ikumbukwe vilevile wasichana hao walisisitiza kwamba wako tayari kwa matokeo hayo na kwamba hawatakubali yawatenganishe.

Je, hatua gani itachukuliwa baada ya matokeo ya DNA

Watoto hao pacha  walipatana baada ya mmoja wao kujifananisha na picha za mwenzake katika mtandao wa kijamii na hata kuibua hisia mseto kufuatia taarifa ya KTN News ambayo iliwaangazia wawili hao.