array(0) { } Radio Maisha | KNUT kimesema hakitaleegza kamba katika kupinga utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi,

KNUT kimesema hakitaleegza kamba katika kupinga utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi,

KNUT kimesema hakitaleegza kamba katika kupinga utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi,

Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT kimesema hakitaleegza kamba katika kupinga utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi, CBC endapo Wizara ya Elimu na Tume ya Huduma za Walimu, TSC hazitakubali kushiriki mazungumzo kuhusu masuala muhimu yanayoikumba sekta ya elimu.

Naibu Mwenyekiti wa KNUT, Collins Oyuu amesema ni jambo la kusikitisha kuona jinsi ambavyo shule nyingi za msingi za umma zinavyoendelea kukumbwa na changamoto ya miundo msingi duni huku zikiendelea kulazimishwa kutekeleza mtalaa huo.

Akizungumzia suala la kufutwa kazi kwa walimu mia mbili themanini wanaoupinga mtaa huo, Oyuu ameishtumu TSC kwa kukiuka sheria zilizopo.  

Kadhalika amepinga uhamisho wa walimu wakuu ambao umekuwa ukiendelea akisema unatatiza utendakazi wao.

Ameyasema hayo wakati wa kongamano la 44 la kila mwaka la walimu wakuu linaloendelea mjini Mombasa huku likiratibiwa kukamilika kesho.