array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Wajir Magharibi, Rashid Kassim akamatwa.

Mbunge wa Wajir Magharibi, Rashid Kassim akamatwa.

Mbunge wa Wajir Magharibi, Rashid Kassim akamatwa.

Mbunge wa Wajir Magharibi, Rashid Kassim akamatwa kwa kumzaba kofi Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Wajir,  Fatuma Gedi. Kassim amekamatwa baada ya Gedi kurekodi taarifa katika Kituo cha Polisi cha Bunge vilevile kupiga ripoti kwa ofisi ya Spika.

Walioshuhidia kisa hicho wanasema Kassim alimshambulia Gedi ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Bajeti kwa kutolitengea eneo bunge lake fedha. Gedi ameeleza kilichojiri.

Kisa cha kushambuliwa kwa mwakilishi huyo wa kike kimechangia vurugu katika majengo ya bunge leo alasiri huku wabunge wanawake wakikishtumu pakubwa. Ilimlazimu Spika Justine Muturi kuwaagiza maafisa wa ulinzi katika bunge kuwaamuru wabunge hao kuondoka ili kutotatiza kikao cha kuwasilishwa kwa makadirio ya bajeti ya mwaka 2019- 2020.  Spika Muturi amewaagiza polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.