array(0) { } Radio Maisha | Waziri wa Fedha, Henry Rotich anaendelea kuisoma bajeti.

Waziri wa Fedha, Henry Rotich anaendelea kuisoma bajeti.

Waziri wa Fedha, Henry Rotich anaendelea kuisoma bajeti.

Waziri wa Fedha, Henry Rotich anaendelea kuisoma bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2019/2020. Rotich anaisoma bajeti hiyo wakati ambapo malumbano yanaendelea baina ya maseneta na wabunge kwa kutokubaliana kuhusu mswada wa ugavi wa mapato, ambao haujapitishwa.

Shughuli ya kusoma bajeti ilitarajiwa kuanza saa tisa alasiri japo imechelewa kwa muda wa takriban dakika arubaini na tano.

Waziri Rotich amesema bajeti ya mwaka wa 2019/ 2020 inalenga kuhakikisha kuwa serikali inafanikisha ajenda zake nne za maendeleo.

Wakati uo huo, amesema kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka minane uchumi wa taifa hili umeendeela kuimarika na unatarajiwa kuimarika hata zaidi mwaka huu.

Aidha, ameeleza mikakati inayotarajiwa kuwekwa na serikali kukabili changamoto mbalimbali ambazo zinaliathiri taifa hili kiuchumi, akitaja kuimarishwa kwa mbinu za kufanyia biashara nchini.