array(0) { } Radio Maisha | Mwakilishi wa Kike wa Wajir, Fatuma Gedi ajeruhiwa.

Mwakilishi wa Kike wa Wajir, Fatuma Gedi ajeruhiwa.

Mwakilishi wa Kike wa Wajir, Fatuma Gedi ajeruhiwa.

Mwakilishi wa Kike wa Wajir, Fatuma Gedi amejeruhiwa baada ya kupigwa kofi na mbunge mwenza katika majengo ya bunge. Gedi tayari amerekodi katika taarifa katika Kituo cha Polisi cha Bunge kwamba alipigwa kofi na Mbunge wa Wajir Mashariki, Rashid Kasim baada ya kuzozana naye kwa muda. 

Inaarifiwa kuwa Kassim alikuwa akitaka kufahamu kwa nini Gedi hakushinikiza Kamati ya Bajeti aliko mwanachama ili eneo bunge litengewe kiasi fulani cha fedha. Mwakilishi wa Kike wa Homaby Gladys Wanga amethibitisha kushuhudia tukio hilo kwani alikuwa akiandamana na Gedi.

Katika picha iliyosambazwa, Gedi anaonekana akitokwa na machozi kadhalika kuonekana kuwa na matone ya damu mdomoni.