array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa watatu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab wafariki dunia.

Washukiwa watatu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab wafariki dunia.

Washukiwa watatu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab wafariki dunia.

Washukiwa watatu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kilipuzi walichokuwa wamekitega kwenye Barabara  ya Bodhai- Bargoni katika  Kaunti ya Lamu.

Maafisa wa usalama wamefawnikiwa kupata bunduki tatu aina ya AK47 kutoka kwenye eneo la tukio.

Tukio hili limejiri siku chache baada ya Kenya kuifunga mipaka yake na  Somalia katika Kaunti ya Lamu kwa sababu za kiusalama.

Aidha kisa cha leo kimejiri takriban miezi miwili baada ya mwanajeshi mmoja wa Kenya kuuliwa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulio la vilipuzi kwenye Kaunti ya Lamu huku gari la maafisa hao likiharibiwa. 

Vilipuzi hivyo vilikuwa vimetegwa ardhini na washukiwa wa Al Shabaab.