array(0) { } Radio Maisha | Adan Duale azungumzia utata unaozingira ugavi wa fedha.

Adan Duale azungumzia utata unaozingira ugavi wa fedha.

Adan Duale azungumzia utata unaozingira ugavi wa fedha.

Huku Waziri wa Fedha, Henry Rotich akitarajiwa kusoma makadirio ya bajeti, Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Adan Duale amezungumzia utata unaozingira ugavi wa fedha kwa kaunti baada ya Bunge la Kitaifa kukosa kuafikiana na Seneti kuhusu kiwango kinachostahili kutengewa kaunti.

Duale amesema kwamba baada ya makadirio ya bajeti kusomwa leo hii, suala la fedha za kaunti bado litaendelea kujadiliwa na kushughulikiwa kwa wakati. Amesema atawasilisha ombi kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kuurejesha mswada wa ugavi wa mapato bungeni wiki ijayo ili ujadiliwe.

Ikumbukwe wabunge wanasisitiza kiwango cha mgao wa kaunti kiwe shilingi bilioni 316 baada ya kuongeza kutoka shilingi bilioni 310 za awali huku seneti ikishuka kutoka shilingi bilioni 335 hadi shilingi bilioni 326