array(0) { } Radio Maisha | Kenya hupoteza shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ufisadi.

Kenya hupoteza shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ufisadi.

Kenya hupoteza shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ufisadi.

Kenya hupoteza kima cha shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ufisadi. Haya ni kwa mujibu wa Balozi wa Marekani humu nchini, Kyle McCarter.

Akizungumza wakati wa hafla moja katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, McCarter amesema cha kushangaza zaidi ni kwamba kiwango hicho cha fedha ndicho Rais Uhuru Kenyatta analenga kukitumia kufanikisha ajenda nne kuu za maendeleo nchini. Amesema licha ya kuimarishwa kwa vita dhidi ya ufisadi, Kenya inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha kupitia ufisadi.

Balozi huyo amewashauri vijana hasa wanafunzi katika vyuo vikuu kushirikiana ili kushinikiza uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.

Kauli yake inajiri siku chache tu baada ya kutoa kauli nyingine iliyofasiriwa kuwa ya kuikejeli hafla ya Maombi ya Kitaifa iliyofanyika jijini Nairobi.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Mcarter aliandika