array(0) { } Radio Maisha | Wakenya wanasubiri kwa hamu kubaini hatua zitakazotangazwa na Wizara ya Fedha

Wakenya wanasubiri kwa hamu kubaini hatua zitakazotangazwa na Wizara ya Fedha

Wakenya wanasubiri kwa hamu kubaini hatua zitakazotangazwa na Wizara ya Fedha

Wakenya wanasubiri kwa hamu kubaini hatua zitakazotangazwa na Wizara ya Fedha ili kupata zaidi ya shilingi bilioni mia sita ambazo ni upungufu katika bajeti ya mwaka 2019/ 2020 ya trilioni 3.02. Inahofiwa kwamba huenda serikali ikatangaza kuongeza kodi kwa bidhaa muhimu mbali na kuomba mikopo ili kuisaidia kuifadhili bajeti ya mwaka huu.

Japo bajeti ya mwaka 2019/ 2020 ni ya chini ikilinganishwa na mwaka 2018/ 2019 kiwanago cha upungufu katika bajeti hiyo ni cha juu kikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na upungufu wa shilingi bilioni mia tano.

Hayo yanajiri huku baadhi ya wabunge wakiitaka Serikali ya Kitaifa kuweka mikakati zaidi ili kuzuia uporaji wa fedha za umma. Wamesema uporaji huo umeathiri matumizi ya fedha za serikali hivyo kuchangia kuongezeka kwa bajeti ya kitaifa kila mwaka wa kifedha. Andrew Mwadime ni Mbune wa Mwatate.

Kwingine wengine wameitaka Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA kuhakikisha kwamba kila mwaka inaafikia viwango vya kodi inayokusanya ili kuisaidia Hazina ya kitaifa kuifadhili bajeti na kuzuia upungufu.

Katika bajeti ya mwaka huu wa kifedha Serikali ya Kitaifa imetengewa jumla ya shilingi trilioni 1.7 katika shughuli zake kukiwapo kuwalipa wafanyakazi wa umma. Kwa upande wao Serikali za Kaunti zimetengewa shilingi bilioni 371.6.  Kwingineno Bunge imetengewa shilingi bilioni 43.6 huku Idara ya Mahakama ikitengewa bilioni 18.9.

Wizara ya Elimu inatarajiwa kuchukua mgao mkubwa zaidi wa bajeti hii, baada ya kutengewa shilingi bilioni 251.7. Sekta ya Miundo Msingi imetengwa shilingi bilioni 186 huku Wizara ya Masuala ya Ndani ikitengewa shilingi bilini 140. Wizara ya Ulinizi imetengewa shilingi bilioni 121.