array(0) { } Radio Maisha | Zephania Okeyo Aura ni miongoni mwa watakao hojiwa IEBC

Zephania Okeyo Aura ni miongoni mwa watakao hojiwa IEBC

Zephania Okeyo Aura ni miongoni mwa watakao hojiwa IEBC

Mmoja wa watahiniwa aliyeibuka wa kwanza wakati wa mahojiano ya kuwatafuta makamishna wa Tume ya Uchaguzi, IEBC ni mmoja wa watahiniwa wengine kumi walioteuliwa kuwania wadhifa wa Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo.

Mapema mwaka 2016, Zephania Okeyo Aura alipata asilimia themanini wakati wa mahojiano ya waliokuwa wakiwania ukamishna japo hakufanikiwa kupewa wadhifa huo. Kwasasa, Okeyo ameratibiwa kuhojiwa tarehe 24 mwezi huu.

Wengine watakaohojiwa ni, Joel Mabonga ambaye aliwahi kuhudumu katika IEBC kabla ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Polisi, na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji Marjan Hussein Marjan. Wengine ni Humprey Okuku Nakitare, Zephania Aura, Mhandidi Christopher Kikoko, Nancy Kariuki, Dkt Murigi Elishibda Muthoni, Dkt Tarus Benjamin, Mwasi Anne Kerubo na Dkt Khalid Billow.

Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji Ezra Chiloba alifutwa na IEBC kwa kukiuka maadili ya kikazo kuabatana na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Edward Ouko ambayo ilitaja tuhuma kadhaa za ufisadi na matumizi mabya ofisi. Chiloba alibebeshwa mizigo yote ya tuhuma zilizoibuliwa na licha ya juhudi zake kutumia mahakama kurejea ofisini hajaweza kufanya hivyo.