array(0) { } Radio Maisha | Sossion aratibiwa kuwahutubia Walimu Wakuu wa shule za Upili
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Sossion aratibiwa kuwahutubia Walimu Wakuu wa shule za Upili

Sossion aratibiwa kuwahutubia Walimu Wakuu wa shule za Upili

Hotuba ya Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Wilimu KNUT Wilson Sossion kwenye Kongamano la Walimu Wakuu wa shule za Upili linaloingia siku ya nne hii leo Jijini Mombasa inatarajiwa kukita zaidi kwenye Mtaala wa Umilisi, CBC.


Sossion ameratibiwa kulihutubia kongamano hilo badaye hii leo huku pia akitazamiwa kuangazia iwapoa kuna hatua zozote zilizopigwa katika mazungumzo yaliyoratibiwa baina ya KNUT, Tume ya Kitaifa ya Huduma za Walimu TSC na Wizara ya Elimu.


Suala la hatua ya TSC kuwafuta kazi walimu wanaoupinga mtaala huo wa sasa vilevile linatarajiwa kushamiri kwenye kinywa cha Sossion.


Jana TSC ilitangaza kuajiriwa kwa walimu zaidi mwaka huu watakaohudumu kwenye Shule za Upili.

Akilihutubia kongamano hilo la 44 la kila mwaka, Mkurugenzi wa TSC Nancy Macharia alisema serikali imetenga shilingi bilioni 2.5 zitakazotumika katika shughuli hiyo ya kuwaajiri walimu elfu tano mwaka huu.

Alitaja walimu wengine elfu tatu pia wataajiriwa kwani serikali imeahidi kutenga shilingi bilioni 1.2 kufanikisha hilo.