array(0) { } Radio Maisha | Maafisa 8 wa KDF wajeruhiwa katika ajali.

Maafisa 8 wa KDF wajeruhiwa katika ajali.

Maafisa 8 wa KDF wajeruhiwa katika ajali.

Maafisa wanane wa Jeshi la Ulinzi la Kenya, KDF wanaendelea kutibiwa katika hospitali mbalimbali ikiwamo ile ya Memorial jijini Nairobi kufuatia ajali ambayo imehusisha lori walilokuwa wakisafiria kwenye Barabara ya Kangundo - Nairobi leo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa eneo la Matungulu - Isaac Thuranera, ajali hiyo imefanyika kwenye eneo la Kamulu wakati lori hilo lililokuwa limewabeba maafisa kumi na wanane, lilikuwa likitoka upande wa Nairobi kuelekea Kangundo na kulikagonga chuma cha daraja na ndipo likaanguka na kuwasababishia wanajeshi hao majeraha.

Thuranera aidha amesema uchunguzi zaidi unafanywa ili kubaini kilichosabisha ajali hiyo.