array(0) { } Radio Maisha | Wazazi wawasihi washikadau wa elimu kuweka kando ubinafsi katika Elimu

Wazazi wawasihi washikadau wa elimu kuweka kando ubinafsi katika Elimu

Wazazi wawasihi washikadau wa elimu kuweka kando ubinafsi katika Elimu

Chama cha Kitaifa cha Wazazi, NPA kimewataka washikadau katika sekta ya elimu kushirikiana na Wizara ya Elimu katika kufanikisha utekelezaji wa Mtalaa wa Umilisi, CBC kwa manufaa ya wanafunzi.

Akiunga mkono msimamo wa Waziri wa Elimu Prof. George Magoha kwa kusisitiza kwamba kamwe hatakubali ombi la wakuu wa shule kuongeza karo, Mwenyekiti wa Chama hicho Nicholas Maiyo amesema wazazi hawatalipa ada za ziada katika karo.

Maiyo amesema wazazi wana imani katika mipango ya serikali kuhusu masuala ya kimasomo, huku akishikilia kwamba wanaopinga mabadiliko ya kielimu wanafanya hivyo kwa manufaa ya binafsi.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Waziri Magoha katika kongamano la walimu wakuu jijini Mombasa, kupinga pendekezo la wakuu wa shule kutaka kuongeza karo kwa madai ya kuboresha viwango vya vya shule zao.

Badala yake Magoha amewawashauri wakuu hao kuafikiana na wazazi na wahisani wengine ambao wako tayari kuchangia katika kuboresha na kuimarisha viwango vya shule zao bila kuweka ada ya ziada katika karo.