array(0) { } Radio Maisha | Maradhi ya Ebola yamuua Mvulana Uganda

Maradhi ya Ebola yamuua Mvulana Uganda

Maradhi ya Ebola yamuua Mvulana Uganda

Mvulana wa umri wa miaka mitano aliyeripotiwa kuambukizwa maradhi ya ebola nchini Uganda amefariki dunia

Mvulana huyo amekufa alipokuwa akitibiwa katika kituo cha afya cha kushughulikia ugonjwa huo kilichoko eneo la Kasese kilomita chache kutoka mpaka baina ya taifa hilo la Jamuhuri ya Kimemokrasi ya Kongo.

Kisa cha kwanza cha Ebola kiliripotiwa nchini humo na Shirika la Afya Duniani, WHO. Wizara ya Afya nchini Uganda imesema wazazi wa mvulana huyo wanafanyiwa uchunguzi ili kubaini iwapo waliambukizwa maradhi hayo.

Marehemu pamoja na wazazi wake walikuwa wamesafiri hadi Kongo kuhudhuria hafla ya mazishi. Mlipuko wa Ebola uliripotiwa Kongo kuanzia mwezi Agosti mwaka jana na watu zaidi ya elfu moja mia tatu wamefariki dunia.