array(0) { } Radio Maisha | Wazazi watakaiwa kukoma kuwaajiri wanao kwenye bodaboda

Wazazi watakaiwa kukoma kuwaajiri wanao kwenye bodaboda

Wazazi watakaiwa kukoma kuwaajiri wanao kwenye bodaboda

Leo ikiwa ni siku ya kukabili ajira za watoto Duniani, tahadhari imetolewa kwa wakazi wa kaunti ya Pokot Magharibi kutowaajiri watoto wa shule kuendesha pikipiki ili kuepuka ajali zinazofanyika kiholelaholela.

Akitoa tahadhari hiyo katika mji wa Makutano, Naibu wa mwenyekiti wa kikundi cha wanabodaboda mjini humo  Simon Kosgei amesema watashirikiana na kamanda wa polisi pamoja na serikali ya kaunti hiyo kukamata na kufunga yeyote atakayepatikana ameajiri watoto.

Kosgei aidha ametoa wito kwa serikali ya Kaunti ya Pokot Magharibi kuwajumuisha vijana wa bodaboda kwenye bajeti ya kaunti ili kuona kwamba vijana hao wamepigwa jeki katika kupata leseni za kuendesha pikipiki.

Ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya waendeshaji pikipiki kaunti hiyo ni wale ambao walikuwa wakiendesha shughuli mbaya ya kuiba mifugo na kwa sasa wamebadili mawazo na kufikiria biashara mbadala, kwa hivyo kuna haja ya serikali kuu na ya kaunti kuzingatia mahitaji yao.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya viongozi wa kaunti ya Busia kulalamikia ajira za watoto katika mpaka wa Kenya na Uganda.