array(0) { } Radio Maisha | Mtoto afariki baada ya kujeruhiwa na lori Mombasa.

Mtoto afariki baada ya kujeruhiwa na lori Mombasa.

Mtoto afariki baada ya kujeruhiwa na lori Mombasa.

Mtoto wa miaka miwili aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General Jijini Mombasa, baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye ajali amefariki dunia.

Mtoto huyo alijeruhiwa baada ya lolri lililokuwa limebeba mchanga kupoteza mwelekeo na kubomoa nyumba yao katika eneo la Kwa Ng'ombe - Aldina Jomvu jana asubuhi.

Ripoti ya matibabu ya hospitali hiyo imeonesha kwamba mtoto huyo alitokwa damu biliwa na hali  kuvuja kwa damu ndani ya kichwa chake Internal Bleeding ambacho kilijeruhiwa vibaya  baada ya kuangukiwa na mawe ya nyumba hiyo.

Jana mama wa mtoto huyo alifariki dunia papo hapo huku babaye pia akijeruhiwa vibaya.

Kamanda wa polisi eneo la Jomvu James Mutua alisema kwamba dereva wa lori hilo lilipoteza mwelekeo baada ya kushindwa kupanda mlima ndiposa likarudi kinyume na kuibomoa nyumba ya watatu hao mwendo wa saa mbili asubuhi.

Wakati wa tukio hilo watatu hao walikuwa ndani ya nyumba hiyo.

Baba na mtoto huyo anaendelea kutibiwa kwenye hospitali hiyo ya rufaa.