array(0) { } Radio Maisha | Mwenyekiti wa KQ Micheal Joseph, ameongezewa muda wa kuhudumu.

Mwenyekiti wa KQ Micheal Joseph, ameongezewa muda wa kuhudumu.

Mwenyekiti wa KQ Micheal Joseph, ameongezewa muda wa kuhudumu.

Siku chache baada ya Afisa Mkuu Mtendaji wa KQ  Sebastian Mikosz kutangaza kujiuzulu,Mwenyekiti wa KQ Micheal Joseph, ameongezewa muda wa kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 4. Michael Joseph ambaye alichukua hatamu mwaka wa 2016, amewashukuru washikadau kwa kuwa na imani naye.

Wiki iliyopita Mikosz alitangaza kujiuzulu mwezi Disemba mwaka huu kabla ya hatamu yake kukamilika mwezi Juni mwaka ujao. Mikosz uamuzi huo wa MIkosz umekashifiwa wengi wakidai kuwa ameshindwa kuleta mabadiliko katika KQ.

Tangazo hilo limetolewa leo wakati wa mkutano wa kila mwaka wa shirika hilo Jijini Nairobi. Vilevile katika mkutano huo Shirika la Ndege la Kenya Airways, KQ limetangaza kusitisha mpango wa kusimamia shughuli za uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.

Michael Joseph aidha amethibitisha kwamba washikadau wa shirika hilo wamepinga mpango wa kumilikiwa na serikali, wakisema awali juhudi zao zilifeli kuendesha shughuli za shirika hilo.

Mapema mwezi uliopita, Mamlaka ya Viwanja vya ndege KAA ilipinga pendekezo la Kenya Airways la kutaka kusimamia shughuli katika uwanja huo kupitia pendekezo la mwekezaji wa kibinafsi.


Ikumbukwe Mwenyekiti wa KAA Isaac Awuondo na Mkurugenzi Mkuu Jonny Andersen waliiambia Kamati ya Bunge ya Uchukuzi kwamba wangewasilisha mapendekezo yao kuhusu namna usimamizi wa uwanja huo unavyoweza kuboreshwa.