array(0) { } Radio Maisha | Watoto watatu wafariki Dunia baada kupigwa risasi.

Watoto watatu wafariki Dunia baada kupigwa risasi.

Watoto watatu wafariki Dunia baada kupigwa risasi.

Watoto watatu wamefariki dunia huku wengine watatu wakilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iten kwenye Kaunti ya Elgeyo Marakwet, baada kupigwa risasi na baba yao usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Marakwet Mashariki Vincent Kitili, amesema mshukiwa aliwafyatulia risasi watoto hao wakiwa wamelala nyumbani kwao katika Kijiji cha Kapker.

Mshukiwa ambaye anadaiwa kuwa mwizi wa mifugo aliwapiga risasi watoto hao ambao wawili ni wake baada ya mzozo kuibuka katika yake na mkewe ambaye hakuwapo wakati wa kisa hicho.

Kitili amesema polisi wanaendelea kumsaka mshukiwa ambaye amekwenda mafichoni. Mili ya watoto hao watatu imepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Iten.