array(0) { } Radio Maisha | Gavana Sang akana madai ya kukamatwa Jijini Kisum.

Gavana Sang akana madai ya kukamatwa Jijini Kisum.

Gavana Sang akana madai ya kukamatwa Jijini Kisum.

Gavana wa Nandi, Stephen Sang amekana madai ya kutiwa nguvuni na hata kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kondele jijini Kisumu.

Akiwahutubia wanahabari muda mfupi uliopita nje ya ofisi yake, Gavana Sang amesema hatua yake ya kuwaongoza wakazi kung'oa miti ya zao la majani chai kwenye shamba linalomilikiwa na kampuni moja ya kimataifa kwenye eneo la Kibwari haijakiuka sheria. Amesema Tume ya Ardhi, NLC kwa ushirikiano na mahakama ilitoa agizo kwamba ardhi inalozaniwa kwenye kaunti hiyo kurejeshewa umma.

Taarifa za awali ziliarifu kwamba Sang alitakiwa kujiwasilisha katika ofisi ya DCI tawi la Nandi Hills kurekodi taarifa kufuatia kisa hicho, la sivyo kibali cha kukamatwa kwake kitolewe.

Hapo jana, ofisi ya Sang ilikana madai kwamba kiongozi huyo yu mafichoni. Baadhi ya viongozi wa eneo la Nandi akiwamo Mbunge wa Nandi Alfred Keter wamekerwa na hatua ya kung'olewa kwa mti wa zao hilo kwenye ekari nne wakisema ni sharti wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.