array(0) { } Radio Maisha | Mtalaa wa Umilisi, CBC kukumbwa na changamoto zaidi

Mtalaa wa Umilisi, CBC kukumbwa na changamoto zaidi

Mtalaa wa Umilisi, CBC kukumbwa na changamoto zaidi

Mtalaa wa Umilisi, CBC unatarajiwa kukumbwa na changamoto hata zaidi baada ya walimu wakuu wa shule za upili kudai kwamba hawajahusishwa katika utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa Kongamano la 44 la Walimu Wakuu linaloendelea jijini Mombasa, Mwenyekiti wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili, KESSHA Kahi Indimuli amesema walimu katika shule za upili hawana ufahamu kuhusu mtalaa huo mpya. Indimuli amesema serikali inapaswa kutoa mwanga wa iwapo mtalaa huo utatekelezwa katika shule za msingi pekee au hata upili.

Aidha, Indimuli amemsihi Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha kuhakikisha washikadau wote wanashirikishwa katika utekelezaji wa mtalaa huo. Aidha, ameiomba serikali kuhakikisha walimu zaidi wanaajiriwa kufuatia idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.

Haya yanajiri huku walimu hao wakisema wataunga mkono mtalaa huo iwapo wataongezewa mshahara. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET Moses Nthurima anasema mtalaa huo utawaongezea kazi walimu, hivyo ni sharti mshahara uongezwe.