array(0) { } Radio Maisha | Wamiliki wa magari Jijini Nairobi wanakabiliwa na changamoto za kulipa ada mpya za kuegesha magari

Wamiliki wa magari Jijini Nairobi wanakabiliwa na changamoto za kulipa ada mpya za kuegesha magari

Wamiliki wa magari Jijini Nairobi wanakabiliwa na changamoto za kulipa ada mpya za kuegesha magari

Wamiliki wa magari Jijini Nairobi wanakabiliwa na changamoto za kulipa ada mpya za kuegesha magari  baada ya Kampuni ya Jambo-Pay kusitisha mkataba wao.

Kwenye taarifa yake, serikali ya Nairobi imetangaza kuchukua jukumu la kukusanya kodi hiyo kuanzia leo, shuhuli ambayo imeonekana kukumbwa na changamoto chungu nzima.

Kwa mujibu wa baadhi ya wamiliki na wahudumu wa magari, changamoto zimeanza kushuhudiwa wengi wakikosa kulipa ada hizo.

Kulingana nao, shughuli ya ulipaji kodi ilikuwa shwari kabla ya kuanza kukwama ilipofika saa moja asubuhi kwani wengi walilipa bila kupata ujumbe wa kuthibitisha malipo yao.

Ikumbukwe kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2014 kampuni ya Jambo-pay ilisaini mkataba na serikali ya kaunti ya Nairobi wa kusaidia kukusanya kodi Jijini.