array(0) { } Radio Maisha | Reuben Nthamburi kufungua kongamano la Walimu wakuu Mombasa.

Reuben Nthamburi kufungua kongamano la Walimu wakuu Mombasa.

Reuben Nthamburi kufungua kongamano la Walimu wakuu Mombasa.

Mkurugenzi wa Tume ya Huduma za Walimu, TSC Reuben Nthamburi anatarajiwa kufungua rasmi Kongamano la 44 la kila mwaka la Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili, KESSHA kwenye kwenye Kaunti ya Mombasa.

Masuala ibuka kufuatia Kampeni kwa jina Last Mile Form one Admission Campaign  towards 100 Percent Transition iliyolenga wanafunzi elfu mia moja thelathini ambao walimaliza darasa la nane mwaka uliopita na hawakuwa wamejiunga na kidato cha kwanza pia yanatarajiwa kujadiliwa kwenye Kongamano hilo.

Mwenyekiti wa Muungano huo Indimuli Kahi amesema kwamba kwenye mjadala huo mapendekezo kuhusu Changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikishuhudiwa kwenye shule za upili kufuatia asilimia kubwa ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu yataangaziwa.

Aidha suala la utekelezaji wa Mtalaa wa Umilisi, CBC linatarajiwa kujadiliwa kwa kina.

Zaidi ya walimu wakuu elfu tisa wanatarajiwa kulihudhuria Kongamano hilo. Kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasimi kesho na Wazriri wa Elimu, Profesa George Magoha.