array(0) { } Radio Maisha | Lonyangapuo amewasuta viongozi wanaoendesha siasa za mwaka wa 2022

Lonyangapuo amewasuta viongozi wanaoendesha siasa za mwaka wa 2022

Lonyangapuo amewasuta viongozi wanaoendesha siasa za mwaka wa 2022

Gavana wa Pokot Magharibi, Profesa John Lonyangapuo amewasuta viongozi wanaoendesha siasa za mwaka wa 2022, akisema wamesababisha kukwama kwa miradi ya maendeleo nchini.

Gavana Lonyangapuo aidha amedai kwamba kuna baadhi ya viongozi kwenye kaunti hiyo ambao wamekuwa wakiwachochea wakazi dhidi yake hasa kwa kumhusisha na ufisadi.

Amesema hatatishwa na viongozi hao kwani ataendelea kutoa huduma kwa wakazi wa Pokot Magharibi.

Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Chepareria, Gavana Lonyangapuo aidha ameahidi kuboresha miundo msingi katika shule hiyo.