array(0) { } Radio Maisha | Pauline Maisy Chesang kufika mahakamani leo.

Pauline Maisy Chesang kufika mahakamani leo.

Kesi dhidi ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Nyeri Pauline Maisy Chesang’ anayedaiwa kushirikiana na wengine wanne kumuua mumewe aliyekuwa Wakili Robert Chesang’ inatarajiwa kuendelea leo katika Mahakama Kuu ya Machakos.

Jaji George Odunga anatarajiwa kutoa uamuzi wa kuwaachilia washukiwa hao watano kwa dhamana lakini kabla ya uamuzi huo, inatarajiwa kuwa Jaji Odunga atasikiliza ombi la dharura ambalo limewasilishwa na familia ya mwendazake Chesang’ wakitaka kesi hiyo ihamishwe kutoka Mahakama ya Machakos na Jaji Odunga ajiondoe.

Familia hiyo inadai kuwa haitapata haki kwani Jaji Odunga alikuwa akisikiliza kesi nyingine zilizowasilishwa na Hakimu Chesang’ na mumewe kabla ya kifo chake, na huenda zikaathiri uamuzi wake.

Kulingana na ndugu wa wakili Chesang’ kwa jina Nehemiah Chesang’ iwapo nduguye hakupata haki katika mahakama hiyo alipokuwa hai, basi hatapata haki hata akiwa marehemu, na hivyo wanataka kesi hiyo ihamishwe katika mahakama nyingine.

Katika kikao cha leo, Jaji Odunga atasikiliza ombi hilo na kutoa uamuzi wake, na iwapo atajiondoa, basi kesi hiyo itawasilishwa mbele ya Jaji Mkuu David Maraga ili aikabidhi mahakama nyingine.

Ikumbukwe kuwa uamuzi wa kuwaachilia washukiwa hao kwa dhamana uliahirishwa katika kikao cha awali wakati hakimu huyo alikosa kufikishwa mahakamani kwa kukosa afisa wa polisi wa kike wa kuandamana naye.