array(0) { } Radio Maisha | CBK yashauriwa kubuni jopo maalum kuwahasisha wananchi kuhusu noti mpya

CBK yashauriwa kubuni jopo maalum kuwahasisha wananchi kuhusu noti mpya

CBK yashauriwa kubuni jopo maalum kuwahasisha wananchi kuhusu noti mpya

Gavana wa Benki Kuu, CBK Patrick Njoroge ameshauriwa kubuni jopo maalumu la kuwahamasisha wananchi kuhusu noti mpya ambazo zimeanza kutumika nchini.

Wito huu umetolewa na wasomi pamoja na viongozi wa kisiasa kwenye Kaunti ya Trans Nzoia ambao wamesema wengi wa Wakenya hasa wakongwe huenda wakalaghaiwa fedha zao iwapo hawatahamasishwa jinsi watakavyobaini noti bandia na halali.

Wakati uo huo, viongozi hao wameshabikia uzinduzi wa noti hizo wakisema utasaidia serikali kulikabili jinamizi la ufisadi nchini. Benson Milimo ni wakili.

Milimo ameridhishwa na uamuzi huo wa serikali akisema itaukabili ufisadi