array(0) { } Radio Maisha | Dula apigwa risasi na maafisa wa Polisi

Dula apigwa risasi na maafisa wa Polisi

Dula apigwa risasi na maafisa wa Polisi

Polisi katika eneo la Kisauni kwenye Kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi kiongozi wa genge la Wakali Kwanza.

Kamanda wa Polisi eneo la Kisauni Julius Kiragu amesema kwamba kiongozi huyo kwa jina maarufu Dula na wanachama wake watatu waliwavamia wenyeji wa Magogoni Kisauni na kuanza kuwahangaisha mwendo wa sanne asubuhi leo.

Kiragu amesema  kwamba polisi waliokuwa wakishika doria waliwaagiza vijana hao kujisalimisha badala yake wakaanza kuwasambulia kwa panga na visu waliyokuwa wamejihami nazo na kuwalazimu polisi kuwafyatulia risasi, Dula akauliwa huku wanachama wake wakafanikiwa kutoroka.

Amesema kwamba tayari mafisa wa polisi wamepata taarifa kuwahusu watatu hao ambayo itawasaidia kwenye msako   huku akiwaagiza kujisalimisha mara moja.

Mwili wa kiongozi huyo wa Wakali Kwanza umelazwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa ya Coast General Jijini Mombasa.