array(0) { } Radio Maisha | Ajiua siku moja baada ya shrehe ya kuzaliwa.

Ajiua siku moja baada ya shrehe ya kuzaliwa.

Ajiua siku moja baada ya shrehe ya kuzaliwa.

Mvulana wa miaka kumi na miwili amejiua siku moja baada ya kufanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa. Mwili wa Brayna Kamuri mwanafunzi wa darasa la sita umepatikana chumbani kwake katika kijiji cha Chagure, Kuanti ya Muranga.

Chifu wa eneo hilo Hannah Wanjiru , amesema kisa hicho ni cha kusikitisha kwani mvulana huyo alijulikana kuwa mwenye furaha na hakuonesha matatizo yoyote. Haijabainika kulichosababisha kisa hicho huku uchunguzi ukianzishwa.

Haya yanajiri wakati ambapo maafisa mbalimbali wamekuwa wakifanya mikutano katika eneo hilo na kuwapa wanafunzi  ushauri nasaha , kufuatia kuongezeka kwa visa vya watoto wadogo kujiua. Hiki ni kisa cha tatu kuripotiwa katika kipindi cha wiki moja kwenye kaunti hiyo.