array(0) { } Radio Maisha | Benard Njiraini ateuliwa kuwa Meneja Mkurugenzi wa KEBs

Benard Njiraini ateuliwa kuwa Meneja Mkurugenzi wa KEBs

Benard Njiraini ateuliwa kuwa Meneja Mkurugenzi wa KEBs

Waziri wa Viwanda na Biashara, Peter Munya amemteua Benard Njiraini kuwa Kaimu Meneja Mkurugenzi wa Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa, KEBs.

Uteuzi wa Munya unajiri miezi miwili tu baada ya bodi ya KEBs kukamilisha shughuli za uchujaji ambapo majina matatu yalitumwa kwake.

Hata hivyo inaarifiwa Waziri Munya hajamteua yeyote miongoni mwa majina aliyotumiwa huku akimteua Njiraini ili kuchukua wadhfa wa Benard Nguyo ambaye muhula wake wa miaka saba umekamilika.

Kwenye barua aliyoandikia wafanyakazi wa KEBs, Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa, Ken Wathome amesema Njiraini aliteuliwa na Munya kushikilia wadhfa huo kikaimu kuanzia tarehe ishirini na saba mwezi uliopita.