array(0) { } Radio Maisha | Viongozi washauriwa kusitisha siasa za mwaka wa 2022.

Viongozi washauriwa kusitisha siasa za mwaka wa 2022.

Viongozi washauriwa kusitisha siasa za mwaka wa 2022.

Viongozi wameshauriwa kusitisha siasa za mwaka wa 2022 ili kufanikisha miradi ya maendeleo kwa Wakenya. Askofu Mkuu wa Kanisa la AIC, Cyrus Yego ameonya kwamba huenda ajenda nne kuu za serikali; Utoshelezo wa Chakula, Makazi Bora, Afya kwa Wote na Ukuaji wa Viwando zikakosa kuafikiwa iwapo siasa zitaendelea nchini.

Kauli ya Askofu Yego inajiri wakati ambapo tayari viongozi wanaompinga Naibu wa Rais William Ruto au kumuunga mkono wakiwa wamejitenga kwa vikundi viwili,  Kieleweke ambacho kinampinga na Tanga-Tanga kinachomuunga mkono kuwania urais mwaka wa 2022.

Akihutubu katika Kanisa la AIC Mwingi, Askofu Yego amewasihi viongozi hao kusitisha siasa ili kufanikisha miradi ya maendeleo nchini.

Wakati uo huo, Yego amesema visa vya ufisadi vimeongezeka katika sekta mbalimbali serikalini hali ambayo inatishia uchumi wa taifa. Askofu huyo amezitaka idara za uchunguzi kuzidisha vita dhidi ya jinamizi la ufisadi nchini.

Hata hivyo Yego amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuhakikisha joto la kisiasa linapungua nchini, huku akimshauri kutokegeza kamba.