array(0) { } Radio Maisha | Dereva wa basi lililosababisha Ajali Naivasha Asakwa na Polisi.

Dereva wa basi lililosababisha Ajali Naivasha Asakwa na Polisi.

Dereva wa basi lililosababisha Ajali Naivasha Asakwa na Polisi.

Maafisa wa polisi Mjini Naivasha , wanaendelea kumsaka dereva wa basi lililosababisha kujeruhiwa kwa watu zaidi ya 60 kwenye  barabara Kuu ya Nairobi -Nakuru

OCPD wa Naivasha, Samwel Waweru amesema dereva huyo anatafutwa baada ya kutoroka.

Aidha Waweru amesema kwamba  abiria kumi na wanane wakiwamo watoto watano wamejeruhiwa vibaya na wanatibiwa katika Hospitali ya Naivasha.

Inaarifiwa sita miongoni mwao wako katika hali mahututi . Abiria hao wanasema dereva wa basi hilo la Mbukinya alikuwa mlevi na alikuwa akiliendesha basi lenyewe kwa mwendo wa kasi.

Mmoja wa abiria kwa jina Kasisi Moses Wafula amesema basi hilo lilitoka mjini Kakamega jana jioni na lilikuwa likija hapa jijini Nairobi.

Hayo yakijiri 

Mtu mmoja amefariki dunia mapema leo kwenye ajali katika Barabara ya Kenol Murang'a karibu na Maragua, huku Waziri wa Maji kwenye Kaunti ya  Murang’a akinusurika kifo kufuatia ajali hiyo.   Ajali hiyo imetokea sehemu ambapo watu watatu walifariki dunia majuma mawili yaliopita.

Kamanda wa Polisi wa Murang’a Josphat Kinyua,  amesema waziri huyo alikua akiliendesha gari lake kwenye barabara hiyo wakati ajali ilitokea.

Kinyua amesema kwamba gari lake lilibingirika alipopoteza mwelekeo na kuugonga mti huku abiria aliyekuwa kwenye gari hilo akifarikia na huku akipata jereha mguuni. Waziri huyo anatibiwa katika Hospitali ya   Murang’a Level Five .

Kamanda huyo amewataka madereva kuwa waangalifu wanapotumia barabara hiyo ili kuepusha visa vya ajali na maafa.