array(0) { } Radio Maisha | Mandago amshauri Buzeki kumuunga mkono Naibu wa Rais

Mandago amshauri Buzeki kumuunga mkono Naibu wa Rais

Mandago amshauri Buzeki kumuunga mkono Naibu wa Rais

Huku Rais Uhuru Kenyatta akiendelea kuwahimiza  viongozi kukomesha siasa za mwaka wa 2022, Gavana wa Uasin Gishu  Jackson Mandago, amewataka wakosoaji wa Chama cha Jubilee kuunga mkono azma ya Naibu wa Rais William Ruto kuwania urais mwaka wa 2022.

Akizungumza kwenye eneo la  Burnt forest , Gavana Mandago amewataka wanaompinga Ruto kumuunga mkono, akisema ana uwezo mkubwa  wa kuutwaa uongozi wa taifa hili wakati wa uchaguzi huo.

Mandago akionekana kumlenga mpinzani wake aliyembwaga kwenye uchaguzi uliopita Mfanyabiashara Zedekiah  Bundotich maarufu Buzeki,  Mandago amesema kwamba Ruto ndiye msemaji wa jamii ya Kalenjin na hivyo anastahili kuuungwa mkono.

Buzeki kwa upande wake, ameikashifu serikali ya Jubilee kwa kuwatelekeza wakulima wa mahindi eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa.   Amesema lazima serikali iweke mikakati  ya kuimarisha kilimo cha mahindi ambacho ni uti wa mgongo wa taifa.