array(0) { } Radio Maisha | Mkewe rais Margaret Kenyatta awashauri Wakenya kutunza mazingira

Mkewe rais Margaret Kenyatta awashauri Wakenya kutunza mazingira

Mkewe rais Margaret Kenyatta awashauri Wakenya kutunza mazingira

Kampuni ya Bidco Afrika kwa ushirikiano na Shirika la Huduma za Wanyamapori, KWS na washikadau katika sekta mbali mbali nchin,  leo wamepanda zaidi ya miche ya mianzi alfu 10,000 katika bwawa la Ruiru Kaunti ya Kiambu.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkewe Rais Uhuru Kenyatta, Margaret Kenyatta ameipongeza kampuni ya Bidco na wote waliyofanikisha hafla hiyo huku akiongeza kuwa ni jukumu la kila Mkenya kuifadhi mazingira.

Aidha amesema kutokana na mvua kubwa inayonyesha nchini  itakuwa  bora iwapo Wakenya watatumia fursa hiyo kupanda miti zaidi ili kuhifadhi mazingira.

Kwa upande wake Vimal Shah Mwakilishi wa Kampuni ya Bidco amesema kampuni hiyo imesambaza zaidi ya  miche millioni moja katika maeneo tofauti nchini na kupanda miche alfu thelathini kufikia sasa.

Shah amesema watashirikiana na washikadau mbalimbali ili kuhifadhi mazingira na kwamba wataendelea na shuguli katika maeneo tofauti nchini ili kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingaira.

Wakati uo huo, Julius Maina ambaye ni afisa wa KWS amesema kampeni hiyo itaendelea ili kuwahamasisha Wakenya kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuongoza shughuli ya upanzi wa miche katika ikulu na kuwataka Wakenya kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Viongozi wengine waliyohudhuria hafla hiyo ni pamoja Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti hiyo Gathoni Wa Muchomba miongoni mwa viongozi wengine.