array(0) { } Radio Maisha | Mswada tata wa jinsia sharti upitishwe,asema Ruto

Mswada tata wa jinsia sharti upitishwe,asema Ruto

Mswada tata wa jinsia sharti upitishwe,asema Ruto

Naibu wa Rais William Ruto amesema Mswada wa Uwakilishi wa Jinsia sharti upitishwe ili kuhakikisha wanawake wanatengewa nyadhfa za uongozi serikalini.

Akihutubu katika eneo la Baragoi Kaunti ya Samburu alipohudhuria mkutano wa amani, Ruto amesema zaidi ya nusu ya wanawake nchini wamebaguliwa hasa katika uongozi , hali inayorudisha maendeleo ya taifa.

Gavana wa kaunti hiyo Moses Lenolkulal kwa upande wake ameiomba serikali kuwarejeshea bunduki maafisa wa polisi wa akiba, NPR  kufuatia kudorora kwa usalama.    Lenolkulal aidha amewashauri wazazi eneo hilo kuwapeleka wanao shuleni, akisema ndio njia pekee ya kupunguza visa vya wizi wa mifugo.   Amesema serikali yake imewekeza pakubwa katika sekta ya elimu , hivyo hakuna sababu ya kutowapeleka watoto shuleni.

Wakati uo huo, Seneta wa kaunti hiyo Steve Lelegwe, amesema usalama umedorora  zaidi, baada NPR kupokonywa bunduki, hali ambayo imesababisha vifo vya watu na mifugo.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Mwakilishi wa Kike katika kaunti hiyo, Maison Leshomo ambaye amemwomba Naibu wa Rais William Ruto kuhakikisha NPR wanarejeshewa bunduki kwa lengo la kudumisha usalama eneo hilo.