array(0) { } Radio Maisha | Rashid Echesa amekigura Chama cha Jubilee na kujiunga na ANC

Rashid Echesa amekigura Chama cha Jubilee na kujiunga na ANC

Rashid Echesa amekigura Chama cha Jubilee na kujiunga na ANC

Aliyekuwa Waziri wa Michezo,  Rashid Echesa amekigura Chama cha Jubilee na Kujiunga na Chama cha ANC.  Echesa ambaye amekuwa na tofauti za kisiasa na Seneta wa Kakamega, Cleophas Malala ,  amesema kwa sasa ataungana naye ili kuhakikisha Kinara wa ANC, Musalia Mudavadi anautwaa uongozi wa taifa hili mwaka wa 2022.

Wakihutubu kwenye hafla ya mazishi katika eneo la Mumias,  wawili hao wamesema wameweka kando tofauti zao za kisiasa ili kufanikisha azma ya Musalia kuutwaa uongozi wa taifa hili.

Wawili hao aidha wamesema kwamba eneo hilo linamunga mkono Mudavadi huku wakiwarai viongozi wengine eneo hilo kuungana.


Kwa upande wake Musalia Mudavadi ,amechukuwa fursa hiyo kumkaribisha rasmi  Echesa katika Chama cha ANC, akisema chama hicho ni cha kitaifa na yeyote anakaribishwa kujiunga nacho.

Mudavadi aidha , amewaomba viongozi nchini kumuunga mkono,  akisema amejitolea kuwasaidia viongozi wakuu nchini kuutwaa uongozi wa taifa.