array(0) { } Radio Maisha | Gavana wa CBK Patrick Njoroge atakiwa kuwahamasisha Wakenya kuhusu noti mpya

Gavana wa CBK Patrick Njoroge atakiwa kuwahamasisha Wakenya kuhusu noti mpya

Gavana wa CBK Patrick Njoroge atakiwa kuwahamasisha Wakenya kuhusu noti mpya

Kiongozi wa Chama cha Ford Kenya, Moses Wetangula ameitaka Benki Kuu, CBK  kuweka mikakati ya kuuhamasisha umma kuhusu vipengee vya katiba vinavyohusiana na fedha ili kuzuia pesa bandia.

Akizungumza katika Eneo Bunge la Kabuchai wakati wa zoezi la uchaguzi wa chama cha Ford Kenya, Wetangula aidha amesema ipo haja ya CBK kubadilisha fedha hizo haraka ili kuepuka wahalifu ambao huenda wakatumia fursa hiyo kuwapora Wakenya.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Mbunge wa Kabuchai, James Mukwe.