array(0) { } Radio Maisha | Ubalozi wa Ufaransa humu nchini umeahidi kushirikiana kuimarisha usalama kwenye fuo za bahari
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ubalozi wa Ufaransa humu nchini umeahidi kushirikiana kuimarisha usalama kwenye fuo za bahari

Ubalozi wa Ufaransa humu nchini umeahidi kushirikiana kuimarisha usalama kwenye fuo za bahari

Ubalozi wa Ufaransa humu nchini umeahidi kushirikiana na Kikosi cha  Walinzi wa Baharini cha Kenya Coast Guards Services ili kuimarisha usalama kwenye fuo za bahari.

Balozi wa Ufaranasa Aline Kuster-Menager amesema tayari ubalozi huo umeweka mikakati na Idara ya Usalama ili kufanikisha shuguli hilo.

Ametaja hatua hiyo kuwa itakayopunguza visa vikiwamo vya ulanguzi wa watu, vile vya dawa za kulevya ambapo vimekuwa vikitekelezwa kupitia fuo hizo.

Kwa upande wake Christine Ribbe ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji kutoka Ufaransa ambacho kiko humu nchini kwa ziara ya siku tano, amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha wanazuru fuo zote za bahari ili kuweka mikakati ya kuimarisha usalama wa baharini.

Jumla ya Wanajeshi kumi na watano waliokuwa wameabiri Meli ya Jeshi la majini kutoka Ufarasa kwa jina Surcouf wamewasili humu nchini mapema leo na kutia nanga kwenye bandari ya Mombasa.

Ikumbukwe manamo mwezi Machi mwaka huu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizuru humu nchini ambapo Kenya na Ufaransa ziliweka mikakati ya kushirikiana ili kifanikisha lengo la Uchumi wa Rasilimali ya baharini Blue Economy.

Awali wakati wa Kongamano la Kimataifa kuhusu rasilimali za baharini Blue Economy lililoandaliwa Jijini Nairobi mnamo tarehe 26 hadi 28 mwezi Novemba mwaka uliopita, Kenya na Ufarasa zilitia saini makataba wa makubaliano kusuhu Usalama wa Ubaharia MASA Agreement