array(0) { } Radio Maisha | Lesuuda ataka serikali za kaunti kulazimishwa kugharamia madeni

Lesuuda ataka serikali za kaunti kulazimishwa kugharamia madeni

Lesuuda ataka serikali za kaunti kulazimishwa kugharamia madeni

Mbunge wa Samburu Magharibi, Naisula Lesuuda sasa anataka serikali za sasa za kaunti kulazimishwa kugharamia madeni. Lesuuda anasema kutokana na malumbanao baina ya viongozi waliotangulia na wa sasa kwenye serikali za kaunti kuhusiana na ni nani wa kuwajibishwa kulipa madeni hayo, sasa anaandaa mswada ambao unalenga kutatua suala hilo ambalo limeathiri hata utendakazi wa serikali ya kitaifa.

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara katika sekta binafsi, wasambazaji wa bidhaa na makundi ya vijana, Lesuuda amelalamikia hatua ya kucheleweshwa kwa malipo ya huduma wanazotoa kutokana na lawama kutoka kwa viongozi walioko serikali na watangulizi wao.