array(0) { } Radio Maisha | Ruto azuru Busia na kutoa ahadi kwa wakazi

Ruto azuru Busia na kutoa ahadi kwa wakazi

Ruto azuru Busia na kutoa ahadi kwa wakazi

Serikali imewaahidi wakazi wanaoshi nyanda za chini kwenye Kaunti ya Busia kwamba imeweka mikakati ya kukabili tatizo la maji na mafuriko. Akihutubu wakati wa ziara eneo hilo, Naibu wa Rais William Ruto amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Sigiri uliogharimu shilingi bilioni 1.2, mradi wa shilingi bilioni 7 wa kujenga ukuta wa kuzuia maji ya mafuriko unaendelea kwenye eneo la Budalang'i na maeneo mengine kwenye Kaunti ya Busia.

Aidha, Ruto amezindua miradi kadhaa ikiwamo ule wa unyunyizaji wa maji mashamba katika nyanda za chini za Nzoia na Sisenye.

Amesema kuwa serikali ya Jubilee itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo, akisisitiza kwamba wakati wa siasa umepitwa na wakati na sasa ni wakati wa kila kiongozi kushirikiana na serikali katika kufanikisha ajenda za maendeleo.

Ruto amesema suala la vyama na siasa halipaswi kuhusishwa katika utendakazi wa viongozi iwapo wanapania kubadili maisha ya wananchi mashinani.