array(0) { } Radio Maisha | Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano la wiki ya mtandao wa kijamii

Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano la wiki ya mtandao wa kijamii

Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano la wiki ya mtandao wa kijamii

Kaunti ya Nairobi inatarajiwa kuwa mwenyeji wa awamu ya nne ya Kongamano la  wiki ya mitandao ya Kijamii maarufu (Social Media Week) kuanzia Jumanne wiki ijayo. Kongamano hilo litakalochukua siku nne litaanza tarehe 11 Juni hadi tarehe 14.

Kongamano hilo linatarajiwa kuwasaidia watakaoshiriki na mawazo na vilevile kubuni nafasi za kujiendeleza sambamba na kuimarisha kampuni zinazotumia mitandao ya kijamii katika kuendesha shuhuli zao.

Baadhi ya wageni mashuhuri watakaohutubu katika Kongamano hilo ni Mkurugenzi wa kampuni ya Turn Left Media Samantha Olivia, Mkurgenzi wa kampuni ya Openworld Limited Dorcus Muthoni, na Sipho Hlela wa kampuni ya Account Executive for East Africa at Meltwater.

Waziri wa Habari na Teknolojia Joe Mucheru na aliyekuwa katibu katika Wizara hiyo Prof Bitange Ndemo pia ni miongoni mwa wageni waalikwa.