array(0) { } Radio Maisha | Wabunge wakashifiwa vikali kwa kutaka marupurupu ya nyumba

Wabunge wakashifiwa vikali kwa kutaka marupurupu ya nyumba

Wabunge wakashifiwa vikali kwa kutaka marupurupu ya nyumba

Wabunge na maseneta wameendelea kushtumiwa kutokana na msimamo wao mkali wa kusema watapinga agizo la mahakama lililositisha hatua ya Tume ya Huduma za Bunge, PSC kuendelea kuwalipa marupurupu ya nyumba. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Haki Afrika limewataja viongozi hao kuwa fisadi na kwamba wanatumia mamlaka yao vibaya. Mkurugenzi Mkuu wa Haki Afrika, Khalid Hussein ametoa wito kwa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC kuwachunguza na kuwachukulia hatua kwa kutaka kujitajirisha kutumia fedha za umma.

Wakati uo huo, amesema iwapo hawatabatilisha msimamo wao basi watalazimika kuyashinikiza mashirika mengine nchini kuandamana.

Wabunge jana waliapa kuyazuia marupurupu ya nyumba ya maafisa wengine wauu serikalini iwapo SRC haitaidhinisha pendekezo lao. si hayo tu walisema kwamba wataipunguza bajeti ya tume hiyo ya mwaka wa kifedha 2019/2020 kwa madai kwamba inawakandamiza na kuwabagua.

Ikumbukwe SRC iliwasilisha kesi mahaamani kupinga hatua ya viongozi hao kulipwa shilingi laki mbil unusu ambazo ni marupurupu ya nyumba, ambapo Mahakama Kuu iliagiza kusitishwa kwa malipo hayo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.