array(0) { } Radio Maisha | Matiang'i apinga vikali uamuzi wa kupunguza miaka ya kuanza kushiriki ngono

Matiang'i apinga vikali uamuzi wa kupunguza miaka ya kuanza kushiriki ngono

Matiang'i apinga vikali uamuzi wa kupunguza miaka ya kuanza kushiriki ngono

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i amepinga vikali uamuzi wa Mahakama Kuu kupunguza miaka ya kuanza kushiriki ngono kutoka miaka kumi na minane hadi miaka kumi na sita. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwazawidi wanafunzi waliotia fora katika Shule ya Upili ya Pangani, Matiang'i amesema kamwe serikali haitakubali kuyaharibu maisha ya baadaye ya watoto ambao wangali shuleni.

Kuhusu suala la michezo ya bahati na sibu, Matiangi amesema ataendelea kuwakabili wafanyabiashara wa michezo hiyo hiyo akisema wanafunzi wengi wameathirika.

Waziri huyo amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa usalama wa aina yote unadumu nchini,huku akidokeza kwmaba amepokea ombi katika wizara yake na kampuni moja ambay hakuitaja ili iruhusiwe kufungua kiwanda cha kutengeneza dawa zinazotokana na bang nchini, ombi ambalo amesema kamwe halitaidhinishwa.