array(0) { } Radio Maisha | Mahakama kuamua kuhusu ombi la kumwachilia Jowie

Mahakama kuamua kuhusu ombi la kumwachilia Jowie

Mahakama kuamua kuhusu ombi la kumwachilia Jowie

Familia ya mfanyabiashara Monica Kimani ambaye uliuliwa, imepinga kuachiliwa kwa dhamana kwa mshukiwa mkuu wa maujia yake Joseph Irungu. Familia hiyo kupitia wakili wake imesema inahitaji muda zaidi kutoa ushahidi kumhusisha Irungu na mauaji ya mwanao.

Familia imesema iliarifiwa wiki iliyopita kuhusu mpango wa kumwachilia mshukiwa kwa dhamana.Mwendesha mashtaka kwenye kesi hiyo Catherine Mwaniki,  amekubali ombi la familia ya marehemu.

Katika uamuzi wake Jaji wa Mahakama Kuu James Wakiaga, ameipa familia hiyo siku saba kujibu kupitia hati kiapo ombi hilo. 

Jowie ambaye amekuwa korokoroni tangu Septemba mwaka jana akihusishwa na mauaji ya Monica Kimani, aliiomba Mahakama kumwachilia baada ya ombi la kwanza kukataliwa kwa msingi kwamba anaweza kutoroka.

Mshukiwa mwengine wa mauaji hayo aliyeshtakiwa pamajo na Jowie ni Mwanahabari wa Runinga ya Citizen Jacque Maribe ambaye aliachiliwa kwa bondi mwaka jana baada ya kukana mashataka. Kesi hiyo itasikilizwa  tarehe 28 Mei.