array(0) { } Radio Maisha | Monicaj Juma azungumzia hatima ya madaktari waliotekwa nyara

Monicaj Juma azungumzia hatima ya madaktari waliotekwa nyara

Monicaj Juma azungumzia hatima ya madaktari waliotekwa nyara

Kwa mara nyingine Wizara ya Masuala ya Nje ya Nchi, imepuuza uwezekano wa mazungumzo kuhusu kikombozi na kundi gaidi la Al Shabaab ili kufanikisha kuachiliwa kwa madaktari wawili wa Cuba ambao walitekwa nyara mjini Mandera mwezi Aprili. Waziri Monica Juma, hata hivyo amesema operesheni inaendelea ili kuwaokoa madaktari hao.

Akizungumza katika kikao na Mwakilishi wa Masuala ya Kigeni na Sera za Kiusalama wa Umoja wa Bara Uropa EU, Federica Mogherini, Juma amesema serikali haiwezi kushiriki mazungumzo na wahalifu na kwamba wawili hao wataokolewa katika operesheni inayoendelea.

Waziri Juma alikuwa akijibu taarifa kuhusu madai ya kundi hilo kutaka kikombozi cha shilingi milioni 150 kutoka kwa Serikali ya Kenya kabla ya kuwaachilia huru kwa madaktari hao.

Juma aidha ameupongeza Umoja wa Bara Uropa kufuatia mazungumzo ya amani huko Somalia kupitia mradi wa kuukabli ugaidi nchini humo. Ameiomba EU kuisaidia Kenya kulitaja Kundi la Al Shabaab kuwa la kigaidi katika orodha yake kuhusu makundi hayo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Uhalifu.