array(0) { } Radio Maisha | mchujo kwa wanaopania kushiriki shindano la East Africa Got Talent limengoa nanga

mchujo kwa wanaopania kushiriki shindano la East Africa Got Talent limengoa nanga

mchujo kwa wanaopania kushiriki shindano la East Africa Got Talent limengoa nanga

Shughuli ya mchujo kwa wanaopania kushiriki shindano la East Africa Got Talent  limengoa nanga rasmi nchini Kenya huku wakazi wa Nairobi wakiatarajiwa kupewa fursa ya kuonesha talanta zao tarehe 1 na 2 mwezi ujao.

Wakazi wa Mombasa walibahatika kuwa wa kwanza baada ya mchujo kuanzia huko wikendi na makundi mbalimbali kujitokeza ili kushiriki.

Waliojitokeza wamepongeza washirika wanaohusia katika kufanikisha  shindano hilo ikiwamo Kampuni ya Safaricom kwa kulenga kujenga vipawa na talanta nchini hasa katika  hali ya sasa ya ukosefu wa ajira.

Kwa mujibu wa Joseph Kusaga ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Tanzania ambapo pia inafadhili amshindano hayo wanawalenga waimbaji, wachekeshaji, wafumba macho na kadhalika katika  mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda. Shindano linatokana na jingine maarufu kote duniani- Americans Got Talent.

Mshindi atatuzwa shilingi milioni 5.