array(0) { } Radio Maisha | Gavana Godana mbele ya Seneti.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Gavana Godana mbele ya Seneti.

Gavana Godana mbele ya Seneti.

Gavana wa Tana River amekuwa na wakati mgumu kueleza matumzi ya fedha za kaunti yake kwa mujibu wa ripoti ya mkagauzi mkuu wa serikali. Godana ambaye alifika mbele ya Kamati ya Uhasibu ya Seneti ikiongozwa na Seneta, Moses Kajwang hakuwaridhisha kabisa maseneta.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mkagauzi Mkuu wa serikali takriban matumizi ya shilingi  milioni 600 hayakuwajibikiwa huku Seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi, akieleza haja ya gavana huyo kuchukua muda zaidi kabla ya kurejea na majibu.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti Moses Kajwang, ambaye pia alishauri kwamba Godana alihitaji kujifahamisha zaidi na maswali yaliyoibuliwa ili kuyajibu.

Seneta wa Narok, Ledama Ole Kina kwa upande wake alimtaka Godana kubeba msalaba wake akitofautiana na wenzake waliotaka apewe muda zaidi.