array(0) { } Radio Maisha | Moses Kuria aishauri Kaunti ya Nyeri, kuwekeza katika viwanda

Moses Kuria aishauri Kaunti ya Nyeri, kuwekeza katika viwanda

Moses Kuria aishauri Kaunti ya Nyeri, kuwekeza katika viwanda

Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria ameishauri Kaunti ya Nyeri,  kuhakikisha kwamba inawekeza katika viwanda kwa kuiga mfano wa kaunti nyingine ambazo zimekeweza pakubwa katika viwanda.

 Akizungumza katika kikao cha kutathmini bajeti ya kaunti hiyo, Kuria amesikitika kwamba, Kaunti ya Nyeri haiwezi kujivunia  kiwanda chochote cha uzalishaji ilichoanzisha.

Kuria ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Bajeti Bungeni, vilevile ameshauri dhidi ya kuhadaiwa kuhusu kuanzishwa kwa miradi mipya ya ujenzi wa barabara,  akisema kwa sasa sera iliyopo ni kukamilisha zile zilizoanzishwa