array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wawili wa wizi wa Biblia, wameshtakiwa

Washukiwa wawili wa wizi wa Biblia, wameshtakiwa

Washukiwa wawili wa wizi wa Biblia, wameshtakiwa

Washukiwa wawili wa wizi wa Biblia, wameshtakiwa katika Mahakama ya Milimani  leo hii. Wawili hao wanadaiwa kuiba Biblia mia nane kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi, washukiwa Reuben Rogoi Maina na John Mapesa Andulu, wameshtakiwa kwa kuwasilisha hundi bandia ya shilingi elfu mia tisa ishirini kwa chuo kimoja  cha Biblia ikiwa malipo ya biblia 800.

Wamekana mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi laki mbili pesa taslimu kila mmoja.