array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Baringo, Kaskazini William Cheptumo alalamikia hali ya usalama eneo hilo

Mbunge wa Baringo, Kaskazini William Cheptumo alalamikia hali ya usalama eneo hilo

Mbunge wa Baringo, Kaskazini William Cheptumo alalamikia hali ya usalama eneo hilo

Mbunge wa Baringo, Kaskazini William Cheptumo amelalamikia hali ya usalama kwenye eneo hilo kutokana na mashambulio mpakani pa Baringo na Pokot.

Akizungumza katika kikao na wanahabari, Cheptumo amemtaka Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dkt. Fred Matiang'i kuchukua hatua sawa na ile ya Matungu na kuhakikisha kwamba wavamiaji wanatiwa mbaroni kwani tayari majina yamewasilishwa kwa vyombo vya usalama.

Cheptumo vilevile amelalamika kuhusu kuondolewa kwa polisi wa kiba licha ya mchango wao katika kudumisha usalama na kutaka maafisa wa kutosha wa usalama kuchukua nafasi zao.

Kadhalika ametaka serikali kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaokwenda shuleni wanapata chakula cha kutosha kwani kufuatia uvamiaji huo,  kadhalika hali ya kiangazi na  njaa imezidi kuwa mbaya.